KIFO CHA MAFISANGO:BOBAN ALIA KAMA MTOTO, KWENDA DRC KUZIKA

 Mshambuliaji wa Timu ya Taifa na Simba, Haruna Moshi 'Boban' akitokwa na machozi wakati wa hafla ya kuaga mwili wa mchezaji mwenzake, Patrick Mutesa Mafisango.Boban ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa marehemu amekuwa akilia kwa uchungu tangu alipopata taarifa za msiba huo akiwa katika kambi ya Stars kiasi cha kushindwa kufanya mazoezi.
Boban ameondoka leo na mwili wa marehemu kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya swahiba wake mkubwa.

 Boban akisaidiwa na mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail Aden Rage wakati akiga mwili wa marehemu Mafisango ambao walikuwa marafiki sana.


 Boban akiwa na majonzi
 Boban akilia kwa uchungu kiasi cha kumfanya akae chini
Boban akifarijiwa na baadhi ya wadau wa Simba

Comments