KAGERA SUGAR KUSUKWA UPYA

KUFANYA vibaya kwenye ligi kuu soka Tanzania Bara kwa timu ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera kumepelekea uongozi wa timu hiyo kujipanga kwa ajili ya kusajili wachezaji mahiri watakaipatia mafanikio timu hiyo kwenye msimu ujao wa ligi.
Kocha Msaidizi wa Kagera Sugar Mrage Kabange amesema kwamba ni lazima wasajili wachezaji wapya na hasa idara ya beki na ushambuliaji.
Ktaika ligi kuu soka msimu 2011/2012 ambayo ilimalizika Mei 6, Kagera Suagar ilimaliza ikishika nafasi ya saba huku Simba ikitwaa ubingwa huo, ikifuatiwa na Azam Fc na Yanga iliyoshika nafasi ya tatu.

Comments