JESHI LA SIMBA LILILOENDA SUDAN HILI HAPA

TIMU ya soka ya Simba inaondoka leo jijini Dar es Salaam kwenda Sudan kwa ajili ya mechi ya marudiano ya michuano ya Kombe la Shirikisho (CAF) dhidi ya timu ya Al Ahly Shandi ya Sudan. Msafara wa Simba utakuwa na wachezaji 19 na viongozi saba. Wachezaji wanaoondoka ni Juma Kaseja, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Derick Walulya, Amir Maftah, Juma Jabu, Obadia Mungusa, Kelvin Yondani, Victor Costa, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Patrick Mafisango, Haruna Moshi, Machaku Salum na Uhuru Selemani. Wengine ni Felix Mumba Sunzu, Emmanuel Arnold Okwi, Edward Christopher Shija na Gervais Arnold Kago. Viongozi wanaofuatana na timu hiyo ni Ismail Aden Rage (MB), Swedy Fikirini Mkwabi, Milovan Cirkovic, Amatre Richard, James Stephan Kisaka, Dk. Cosmas Kapinga, Nicholaus Menrad Nyagawa na Ezekiel Kamwaga. Mkuu wa msafara huo atakuwa ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Hussein Mwamba. Wachezaji wawili; Nassor Said Masoud (Chollo) na Juma Said Nyoso hawatakwenda Sudan kwa vile wanatumikia adhabu zao za kukosa mechi kutokana na kuwa na kadi. Mechi ya Shandi na Simba itapigwa Jumapili ijayo katika Uwanja wa Shandi wenye uwezo wa kuchukua washabiki 10,000. Mji wa Shandi uko Kaskazini Magharibi mwa Sudan na uko umbali wa kilomita 150 kutoka mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.

Comments

  1. ALL THE BEST SIMBA SPORTS CLUB, HOPE TO EARN MORE OF WHAT THEY HAVE PLANTED FROM THE LAST MATCH.

    ReplyDelete

Post a Comment