FRANCIS KIFUKWE KURITHI MIKOBA YA NCHUNGA?

SIKU chache baada ya mwenyekiti wa Yanga Lloyd Nchunga kumwaga manyanga, imeelezwa kwamba nafasi yake huenda ikarithiwa na aliyepata kuwa rais wa timu hiyo, Francis Mponjoli Kifukwe.
Habari zilizopatikana kutoka Yanga zinadai kuwa wazee wa klabu hiyo ambao walishiriki kwa kiasi kikubwa katika kushinikiza Nchunga ajiuzulu kutokana na kushindwa kuingoza vema timu hiyo, wamempa jukumu Kifukwe kusimamia timu hiyo.
Kifukwe amnbaye aligombea na Nchunga katika uchaguzi wa mwaka 2010 kabla ya kujitoa ni mmoja ya wajumbe wa bodi ya udhamini ya klabu hiyo sambamba na Mama Fatma Karume, Yusuf Manji, Deo Filikunjombe na  Abas Mtemvu.
Hata hivyo huenda zoezi hilo likakwama kwani kamati ya sheria, maadili na hadhi za wachezaji ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) chini ya mwenyekiti wake Alex Mgongolwa, imeanza kushughulikia suala la mgogoro huo.
Hiyo inafuatia kamati ya uchagfuzi ya Yanga kuomba mwongozo juu ya mustakabli mzima wa uongozi baada ya kolamu yake kutotimia kwani tayari ku na baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji walimwaga manyanga.
Aidha, baraza la wazee nalo lilidai kuwa kwa sasa hakuna kiongozi kwani Nchunga amejiuzulu na wenzake wote.

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHMay 26, 2012 at 11:23 PM

    KIFUKWE SIKU ZOTE NDIO CHANZO CHA MIGOGORO YA YANGA NA NDIO AMEKUA AKIONGOZA MAPINDUZI YA VIONGOZI HALALI KLABUNI HAPO KWA KUJIFICHA NYUMA YA WANACHAMA WANAOJIITA MAARUFU WA YANGA NA HAO WAZEE NJAA AMABO WENGI ANAWAMUDU,WENYE AKILI SIKU NYINGI TULIJUA HII NI KAZI YA KIFUKWE KWANI MANENO ALIYOTAMKA PTA SIKU YA UCHAGUZI WAKATI ANATANGAZA KUJITOA KATIKA UCHAGUZI BAADA YA KUONA DALILI ZA KUSHINDWA NA LOYD NI KWAMBA MTOTO "AKILILIA WEMBE WACHA UMKATE"AKIIMAANISHA MTOTO NI LOYD NA KWELI AMETIMIZA LENGO LAKE.ALIWAHI KUFANYA HIVI KWA TARIMBA NA MALINZI PIA,HATA WALE YANGA ASILI MLIOKUWA MKIWASIKIA WAKIMSUMBUA TARIMBA NA BAADAE MALINZI ALIKUA NI YEYE HUKU AKIJIFANYA NI MMOJA WA VIONGOZI WANAOPINGWA NA YANGA ASILI KUMBE NI USANII WAKE TU.

    SAYZ MDAU WA BOMBA,BOSTON,MASSACHUSSETS

    ReplyDelete

Post a Comment