FM ACADEMIA, KHADIJA KOPA KUPAMBA MISS KURASINI 2012


WAKATI shindano la kumsaka Redd’s Miss Kurasini 2012 likitarajiwa kufanyika keshokutwa  kwenye ukumbi wa Equator Grill uliopo Mtoni jijini Dar es Salaam, mrembo atakayetwaa taji hilo atazawadiwa kitita cha sh.500,000. 
Mkurugenzi wa Zum Fashions and Entertainment inayoandaa shindano hilo Zuwena Mustapha, alisema kwamba maandalizi ya shindano hilo yanaendelea ambapo warembo 16 watapanda jukwaani kuwania taji hilo. 
Alisema mshindi wa pili ataondoka na sh.350,000, huku mshindi wa tatu atapata sh.250,000, wakati mshindi wa nne na wa tano kila mmoja atapata sh.200,000 na washiriki waliosalia kila mmoja atapata sh.200,000. 
Zuwena aliongeza kuwa warembo hao wanaendelea na mazoezi katika ukumbi huo chini ya ukufunzi wa mshindi wa taji la vipaji katika fainali za Miss Tanzania mwaka 2011 Rose Herbert.Taji la Miss Kurasini linashikiliwa na  Mwajabu Juma ambaye pia anashikilia taji la Top Model la Miss Tanzania mwaka 2011. 
Aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Tulekene Seth, Christina Moses, Flaviana Maeda, Farida Mrope, Edina Magige, Nzelani Juma, Anna Zakaria, Linda Deus, Angle Gasrper, Zuhura Sadiki, Mwanaisha Zuberi, Irene Sostenes, Sia Kimambo, Lilian Joseph, Asha Musa na Betty Peter. 
Aidha, bendi ya  muziki wa dansi ya Fm Academia na malkia wa taarab nchini Khadija Omar Kopa wanatarajiwa kupamba fainali za shindano la Miss Kurasini mwaka 2012 zitakazofanyika kesho kwenye ukumbi wa Equator Grill, uliopo Mtoni Sabasaba jijini Dar es Salaam. 
Miss Kurasini imedhaminiwa na Lady Pepeta, Flexip, Redd’s, Pj Amusement, Dodoma Wine, Renzo Salon, Madirisha Video Production, Jambo Leo, Aucland Tours and Safaris, Clouds Fm, Father Kidevu Blog, Candy Bureau de Change, Neema Classic Wear na Giraffe Ocean View Hotel.

Comments