FERGUSON KUTUA NA ZAWADI KIBAO KWA MASHABIKI WA MASHUJAA MUSICA


MWANAMUZIKI wa bendi ya muziki wa dansi ya Mashujaa, Saulo John ‘Ferguson’. aliyekuwa mapumzikoni nchini Afrika Kusini anatarajiwa kurejea nchini kesho  asubuhi na usiku ataanza kufanya vitu vyake kwenye ukumbi wa San Siro.
Meneja wa hiyo King Dodoo la Buche, alisema kuwa mwanamuziki huyo aliyekuwa mapumzikoni nchini humo anarejea na kuanza kazi yake kesho ambapo anatarajiwa kurudi na vitu vipya kutoka nchini huko
 Alisema katika onesho hilo Furguson atatumia nafasi hiyo kuwaonjesha vionjo vypya alivyotunga akiwa nchini humo.
 Naye Furguson ambaye alizungumza kwa njia ya simu akiwa nchini huko ‘Ferguson’ katika mapumziko hayo ameweza kupata mawazo ya kubuni rapu mpya ambazo zitaanza kutumika katika bndi yake hiyo.
 Ferguson alisema amejipanga kuanza kuonesha rapu hizo wiki hiyo kuanzia katika onesho lake la kwanza ambalo litafanyika katika ukumbi wa SunSiro siku ya Alhamis.
 Alisema kuwa katika ziara yake hiyo ya nchini Afrika Kusini ilikuwa na mafanikio makubwa licha ya kuwepo ukweni. 
"Nilikuwa nimeenda ukweni kwangu...lakini nimepata vitu vipya ambavyo tutavifanya  na wanamuziki wenzangu wa Mashujaa na kuleta mabadiliko makubwa katika bendi yetu"alisema Ferguson.
 Ferguson, alisema kwa kutambua mchango wa wanamuziki wenzake katika kuleta mabadiliko katika soko la muziki wa ndansi hapa nchini watakaa na kuangalia wafanye nini zaidi ili bendi yao iweze kuja kivingine.
 Hivi karibuni bendi hiyo ilipata wanamuziki wapya, ambao ni Sudi Mohamed ‘MCD’, Charles Gabriel ‘Chalz baba’, Lilian Tungalaza Internet, na Ally Akida kutoka bendi ya Twanga Pepeta. 
Mashujaa Ijumaa itakuwa na onesho lake katika ukumbi wa Business Park uliopo Kijonyama wakati Jumapili jioni itakuwa kwenye Bonanza la kila wiki kwenye viwanja vya TCC Club Chang'ombe.

Comments