FERGUSON AJA KIVINGINE MASHUJAA MUSICA





MWANAMUZIKI wa bendi ya muziki wa dansi ya Mashujaa, Saulo John ‘Ferguson’. aliyekuwa mapumzikoni nchini Afrika ya Kusini atarejea Jumatano akiwa na rapu mpya zitakazotumika katika bendi hiyo.
Akizungumza kwa njia ya simu akiwa nchini huko ‘Ferguson’ katika mapumziko hayo ameweza kupata mawazo ya ubuni rapu mpya ambazo zitaanza kutumika katika bndi yake hiyo..
Ferguson alisema amejipanga kuanza kuonesha rapu hizo wiki hiyo kuanzia katika onesho lake la kwanza ambalo litafanyika katika ukumbi wa SunSiro siku ya Alhamis.

Alisema kuwa katika ziara yake hiyo ya nchini Afrika Kusini ilikuwa 

na mafanikio makubwa licha ya kuwepo ukweni.na wakwe zake nchini  humu ambapo amekaa kwa muda wa 

siku 10.

Ferguson, alisema kwa kutambua mchango wa wanamuziki 

wenzake katika kuleta mabadiliko katika soko la muziki wa ndansi 

hapa nchini watakaa na kuangalia wafanye nini zaidi ili bendi yao 

iweze kuja kivingine.

Hivi karibuni bendi hiyo ilipata wanamuziki wapya, ambao ni Sudi 

Mohamed ‘MCD’, Charles Gabriel ‘Chalz baba’, Lilian Tungalaza 

Internet, na Ally Akida kutoka bendi ya Twanga Pepeta.

Mashujaa Ijumaa itakuwa na onesho lake katika ukumbi wa 

Business Park uliopo Kijonyama wakati Jumapili jioni itakuwa 

kwenye Bonanza la kila wiki kwenye viwanja vya TCC Club 

Chang'ombe.

Comments