ESTHER BULAYA CUP YAFIKIA TAMATI

MBunne wa Viti Maalum Vijana (CCM)Esther Bulaya akikabidhi zawadi kwea mabingwa wa michuano aliyoiandaa ya Esther Cup ambapo timu ya Town Star ilitwaa ubingwa. Michuano ya Mbunge wa Viti maalum kupitia Umoja wa vijana CCM mkoani mara ESTHER BULAYA CUP imemalizika jana ambapo michuano hiyo imedumu kwa wiki mbili katika wilaya Bunda mkoani Mara,Katika michuano hiyo Mshindi alikuwa ni Town Star baada ya kuifunga timu ya Amani FC mabao 4-2 kwa mikwaju ya Penalti Huku mshindi wa tatu Ikiwa Timu ya Polisi Fc Katika michuano hiyo Town Stars walipata zawadi ya shilingi 500000 na kombe, huku amani iliyokuwa ya pili ilipata shilingi 250,000 na Polisi Fc iliyoshika nafasi ya tatu iliondoka na shilingi 150,000 Aidha, mchezaji bora alikuwa Ramadhani Kifundu kutoka Aman Fc aliyepata zawadi ya shilingi ya shilingi 50,000, huku Mfungaji bora kutoka timu ya Balili fc alipata shilingi 50,000 na Mwembeni Fc ilipata shilingi 50,000 kutokana na kuwa timu yenye nidhamu.

Comments