DULLY SYKES, CHID BENZ KUPAMBA SHINDANO LA KUSAKA VIPAJI VYA UBUNIFU CHIPUKIZI WA MITINDO MKURUMAH HALL KESHO

The creative Entrepreneur Mustafa Hassanali, talking to the media during the Media briefing of the INDIAFRICA A Shared future programme. INDIAFRICA: A Shared Future kwa ajili ya watu bilioni mbili. Mpango maalumu wa nchi ya India wa kukuza mbinu za ushirikiana wa kinaendeleo baina ya India na Afrika Kwa mujibu wa Balozi Pinak Chakravarty, Katibu Maalumu wa idara ya Umma ya Wizara ya Mambo ya Nje na Diplomasia "India na Afrika tunaingia katika ukurasa mpya baada wa kihistoria kupitia ukoloni na unyonyaji wa kiuchumi hadi kufikia uhuru. Na sasa uhusiano wetu unazidi kukua kwa kasi. Uhusiano wetu huu mpya umeegemea zaidi katika uhusiano wa kiuchumi katika dunia hii ya utandawazi. theIdeaWorks, ni mpango maaalumu wa kibiashara ambao makao makuu yake yako mjini Delhi, na unasimamiwa na idara maalum ya Umma, chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya serikali ya India. INDIAFRICA: A Shared Future ni mpango wa miaka mitatu na ulizinduliwa mnamo mwaka 2011. Mpango wa P2P inakaribisha mbadilishano wa mawazo kati ya vijana kutoka Africa na India, kupitia mfululizo wa mashindano mbalimbali ya wajasiriamali vijana. Pia ina lengo la kujenga jukwaa la vijana wajasiriamali kutoka India na Afrika lenye nguvu, uvumbuzi na ushindani. "Kuongezeka kwa uwezo wa kiutamaduni, ni muhimu kwa ajili ya mafanikio, Na kuwajenga vijana kuwa raia wazuri wa kimataifa na kukuza ndoto na matarajio yao katika nchi yoyote duniani. Kwa mtazamo huu, watu hasa vijana wana jukumu kubwa na muhimu la kujenga dunia na kushikamana ili kuweza kuleta maisha bora kwa watu wote baadae, ikiwa watu wote bilioni mbili wakijenga ndoto na historia yao kwa pamoja." Alisema Seema Kundra, Mkurugenzi wa theIdeaWorks. INDIAFRICA:A Shared Future ni mpango wa kimawasiliano unaojumuisha mashindano mbalimbali kama, uandishi wa insha, upigaji picha na ubunifu. Hii itasaidia kujenga jukwaa la vijana kutoka Afrika na India wenye vipaji na uwezo wa kushirikiana katika changamoto na mafanikio yao; Na baadae kushirikiana kiubunifu, biashara na utamaduni. Jumuia ya vijana wenye malengo na mipango ya kubainisha wajasiriamali vijana kutoka India na Afrika, na unawapa fursa ya ukuaji na ushirikiano. Lengo lake ni kubadilishana mawazo na kuongeza uelewa mzuri wa changamoto na fursa za kibiashara katika pande zote mbili. Nikimnukuu Navdeep Suri, Katibu Mkuu wa Idara ya Diplomasia na Umma, Wizara ya Mambo ya Nje ya India alisema, "70% ya idadi ya idadi ya watu katika bara la Afrika kwa sasa wako chini ya umri wa miaka 25, ambapo ni takwimu zinazoshabiihana na India. Hivyo basi ni muhimu sana kukuza ushirikiano kati ya vijana kutoka Afrika na India ili kusafisha njia kwa ajili ya malengo ya pamoja hapo baadae. Lengo la mpango huu ni kufanya kazi kwa pamoja ili kuibua nishati hiyo kubwa ya vijana na kuhamasisha mawazo yao ya kipekee na yenye nguvu na ubunifu, na kuwawezesha kuwa wawezeshaji na vichocheo vya mchakato huo." Katika kila kila kundi la ushindani, zawadi ya fedha taslimu ya Dola 1000 za Kimarekani kwa washindi watatu kutoka kila kanda ambazo ni Afrika Mashariki,Afrika Magharibi,Afrika ya Kati,Kusini na India. Kila mshindi wa shindano la vijana wenye maono, watapewa ziara ya siku tano kati ya India au Afrika (kulingana na nchi aliyopo) ambayo itaambatana na semina na mikutano ya kibiashara; Pamoja na muingiliano ya kimawasiliano ya kibiashara. Washiriki wachache wa mwisho watakaotajwa wataweza kushiriki katika shindano la dola 10,000 za Kimarekani na kuendeleza ushirikiano kati ya India na Afrika. INDIAFRICA itasaidia kuvunja mipaka na kukuza na kuhamasisha ushirikiano mpya, na utambuzi wa kimataifa na kutatua matatizo ya kirasilimali kati ya wanafunzi wa vyuo vikuu, shule za sekondari,sekta ya viwanda, wajasiriamali na viongozi kutoka India na Afrika ili kuweza kuukaribisha mpango huu wa INDIAFRKA. Hivyo kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambao kwa sasa wanasherehekea miaka 50 ya kuanzishwa kwake pamoja na AIESEC Tanzania,INDIAFRICA imeandaa kongamano linalojumuisha vyuo vyote litakalofanyika mnamo tarehe 12 Mei 2012 katika ukumbi wa Nkuruma ndani ya chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kongamano hili ni bure kabisa kwa wanfunzi wote wa elimu ya juu, wataalamu na vijana. Washiriki wote watapata nafasi ya kubadilishana mawazo na wajasiriamali vijana kutoka India na Tanzania. "Mpango huu ni jukwaa kamili la kwa ajili ya wajasiriamali vijana, kwa ajili ya kuandaa matarajio yao ya baadae ya kazi zao. Maendeleo yetu ya kesho, yamo mikononi mwa kijana wa leo, nami nimepata heshima ya kuwa sehemu ya mradi huu ambao una lengo la kuleta India na Afrika kwa pamoja hasa Tanzania ; Kuimarisha mahusiano ya nchi hizi mbili kwa karne mbili" Alisema Mustafa Hassanali mbunifu nguli wa mavazi Tanzania na muandaaji wa Swahili Fashion Week. Swahili Fashion Week kwa pamoja na INDIAFRICA wanaandaa mashindano maalumu kwa ajili ya kuleta muingiliano kwa vijana wadogo wanaochipukia katika nyanja ya ubunifu wa mitindo nchini Tanzania, ambapo washindi wataweza kuonyesha ubunifu wao katika maonyesho makubwa ya mavazi Afrika mashariki na kati ya Swahili Fashion Week yanayofanyika mwezi November kila mwaka. "Tunatoa wito mkubwa kwa kila mtu kushiriki katika mdahalo huu wa aina yake hapo tarehe 12 Mei 2012,ambapo hautapata nafasi ya kukutana na vijana wajasiriamali wenye maono ya mafanikio na maendeleo tu, bali pia hafla fupi ya muziki itakayofanywa na wasanii wanaotikisa nchini Tanzania," Alihitimisha Seema Kundra Kuhusu INDIAFRICA: A Shared Future Mpango wa INDIAFRICA umezaliwa nje ya utambuzi wa hisia za pamoja ili kuweza kuunganisha historia na tamaduni kati ya India na Bara la Afrika, na uhusiano wa Wahindi zaidi ya milioni mbili waishio nje ya India. Pia INDIAFRICA imedhamiria kutoa jukwaa kwa wanafunzi, wafanyabiashara vijana na watu mbalimbali wenye maono ya mbali kupitia midahalo ya pamoja.Pia kushirikiana kwa pamoja katika Nyanja ya kibiashara na ubunifu, mpango wa INDIAFRICA ni mpango wa muda mrefu unaoendelea ukizingatia historia na uhusiano kati ya India na Afrika Kuhusu theideaworks TheIdeaWorks, ni mpango pekee wa mawasilino nchini India ambao unasimamia miradi ya umma ya kidiplomasia.Kupitia ushirikiano na makampuni makubwa ya kibiashara, taasisi za serikali, na wanajiografia, theIdeaWorks inaendelea na mipango mbalimbali ya kimaarifa na mahusiano katka miradi mbalimbali.

Comments