CFAO MOTORS YASAIDIA KUFANIKISHA MASHINDANO YA MCHEZO WA KUOGELEA TANZANIA

Baadhi ya washiriki wa mashindano ya kuogelea wakichumpa kwenye maji.
Baadhi ya Mashabiki wa mchezo wa kuogelea waliohudhuria mashindano hayo.
Time Keepers wakihakikisha washindi wanapatikana kihalali.
Makocha, wazazi na wanamichezo wakisubiri kutajwa kwa washindi wa mashindano ya kuogelea yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa Juma.
: Time Keepers waliosimamia shindano hilo wakipungia mashabiki.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Bw. Alfred Minja akiwavisha medali baadhi ya washindi wa mashindano ya kuogelea yaliyofanyika katika Shule ya Hopac iliyopo jijini Dar es Salaam. Na.Mwandishi wetu Kampuni na taasisi mbalimbali nchini Tanzania zimepewa wito wa kusaidia udhami wa kusaidia mashindano yajayo ya kuogelea ili washiri waweze kuwakilisha vyema na kuitangaza Tanzania. Akizungumza na Mwandishi wetu Mkurugenzi wa Ufundi wa Chama hicho Bw. Marcelino Ngalioma ambaye ameandaa mashindano kuogelea kwa vilabu vyo te vya Tanzania, amesema mashindano hayo mwaka huu yamefanikiwa sana ambapo vilabu 250 vimeshiriki. Amesema mwaka huu mashindano hayo yameonyesha mafikio makubwa kwa kuwa mara ya mwisho kulikuwa na washiriki 170 pekee, lakini sasa wamepata washiriki kutoka mikoa ya Mwanza, Arusha, Mwanga, Moshi, Morogoro, Zanzibar na dare s Salaam. Aidha Bw. Ngalinoma ametoa shukrani za dhati kwa kampuni inayojishughulisha na usambazaji wa magari ya NISSAN ya CFAO Motors kwa kutoa udhamini ikiwa ni pamoja na kuhahakisha mchezo huo unakuwa hapa nchini. Pia amesema hivi karibu chama hicho kitarajia kuwa na kambi maalum kwa ajili ya wachezaji wake (Residential Camp) kwa muda wa mwezi mzima wakijiandaa kwa mashindano yatakayofanyika Nairobi nchini Kenya. Amefafanua kuwa Mashishindano hayo ni kwa Arika nzima na yatakayoshirikisha vijana na pia kutakuwa na mashindayo ya wazi (Open Chmpionship) yatakayofanyika kuanzia mwezi Septemba tehe Mosi na terehe 2. Vilevile amesema wakati huo huo watakuwa wanamuandaa mwogeleaji mmoja anaitwa Magdalena Moshi anayekwenda kushiriki michuano ya Olimpiki ikiwa ni pamoja na kufanya mafunzo mikoani ili kuhakikisha mchezo huo unaendelea nchi nzima. Katika kuunga mkono maendeleo ya mchezo huo kampuni ya CFAO Motors imeamua kutoa mchango wake kwa kudhamini mashindano hayo kwa kuwa imeona ni mchezo wenye manufaa kimichezo na kiafya na huenda ukafanikiwa kulitangaza taifa tofauti na michezo mingine ambapo kampuni kadhaa zinawekeza lakini matunda hayaonekani. Akizungumza Mkurugenzi wa Masoko wa CFAO Motors Bw. Alfred Minja amesema kampuni hiyo inakusudia kufanya mazungumzo na chama hicho na kuangalia njia watakazo tumia kuwalea na kuwaendeleza wachezaji wa mchezo huo.

Comments