BERKO HUYOOO AZAM FC

KIPA wa kimataifa wa Yanga Mghana Yaw Berko huenda msimu ujao wa ligi akaidakia klabu ya soka ya Azam. Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana zinaeleza kwamba Berko amefiklia uamuzi wa kuipa kisogo Yanga baada ya kupoteza namba katika kikosi hicho kutokana na maumivu. Aidha, kama mambo yakienda vema Azam pia itawang'oa Yanga nyota wake Haruna Niyonzima na Nadir Haroub 'Canavaro'l

Comments