BENCHI LA UFUNDI YANGA NALO LAJIVUA GAMBA

Aliyekuwa kocha msaidizi wa YAnga Fred Felix Minziro wa kwanza kulia na viongozi wengine wa benchi la ufundio la Yanga ambao jana walitangaza kujitoa katika klabu hiyo. BENCHI zima la ufundi Yanga limeachia ngazi, ili kutoa shinikizo la kulipwa madai yake- ambayo ni malimbikizo ya posho na mishahara. Kaimu Kocha Mkuu, Freddy Felix Minziro na kocha wa makipa, Mfaume Athumani Samatta wameserma leo kwamba hawataanza kazi Juni 1, mwaka huu kuandaa kikosi kwa ajili ya michuano ya Kombe la Kagame, ambayo klabu hiyo ni bingwa mtetezi hadi walipwe mafao yao. Kwa sasa Yanga kuna mgogoro na migomo, ambayo lengo lake ni kumshinikiza Mwenyekiti wa klabu hiyo, Wakili Lloyd Baharagu Nchunga aachie ngazi. Jana Nchunga aliiambia BIN ZUBEIRY kwamba vita anayopigwa ni kubwa na imefikia wakati hadi anahofia usalama wake, kwani anahisi watu wanaweza kumdhuru ili kutimiza nia yao ya kuhakikisha hayupo Yanga. "Nafikiria mara mbili kama kuna haja ya kuendelea kuhatarisha maisha yangu kiasi hiki, maana ilipofikia mtu anaweza kupewa fedha akaja hata kuniua, isitoshe nguvu ya fedha inayotumika katika vita hii ni kubwa sana, kiasi kwamba sielewi chanzo chake ni nini,"alisema.

Comments