BAADA YA KAULI NZITO TOKA KWA WAZEE WA YANGA HATIMAYE NCHUNGA AKUTANA NA KAMATI YA UTENDAJI YA YANGA KUJADILI CHA KUFANYA

Mwenyekiti wa Yanga Lloyd Nchunga akiwa na baaadhi ya wajumbe wa kamati ya Utendaji ya Yanga Mohammed Bhinda, Tito Osoro na Katibu wa klabu hiyo Mwesiga Selestine walipokitana leo katika hoteli ya Courtyard jijini Dar es Salaam
Msemaji wa Yanga Louis Sendeu aliyesimama akizungumza mawili matatu na viongozi wenzake wa Yanga. BAADA ya makundi na kada tofauti ndani ya klabu ya Yanga kuelekezxa makombora kwa uongozi wa timu hiyo ikishinikiza ujiuzulu kutokana na timu hiyo kuonyesha mwenendombaya katika ligi kuu soka Tanzania bara na hatimaye kuutema uningwa, hatimaye uongozi umekutana kwa ajili ya kujadili hali tete inayoendelea ndani ya klabu hiyo. Mwenyekiti wa Yanga na kamati ya utendaji hivi karibuni ilijikuta katika msigan o na wazee wa baraza poamoja na wanachama wakiwataka kuachia ngazi baada ya kushindwa kuiletea mafanmikio, hatua ambayo uongozi ulidai si suluhisho la matatizo yaliyopo na kwam,ba ungekutana kujadili na kujua cha kufanya. Kama hiyo haitoishi hasira za wanachama hizo zilizidi baada ya timu kuchjapowa mabao 5-0 na mahasimu wao wa jadi Simba katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu soka Tanzania bara.

Comments