AZAM NA MTIBWA KURUDIANA

Wachezaji wa Mtibwa
KAMATI ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shiriksho la Soka Tanzania (TFF) imeamuru mchezo kati ya Azam FC uliovunjika zikiwa zimesali dakika chache, timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1 wiki mbili zilizopita kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi, Dar es Salaam urudiwe.
Habari ambazo BIN ZUBEIRY imezipata kutoka kwenye kikao cha Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Kamanda Mstaafu, Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, Alfred Tibaigana kilichofanyika jioni ya leo Dar es Salaam, zimesema kwamba mchezo utarudiwa kwa sababu imebainika makosa yalikuwa ni ya waamuzi na si Mtibwa.
Kama imebaini waamuzi hawakufuata kanuni za kusubiri kwa dakika 10, wakati wachezaji wa Mtibwa Sugar wamegoma kabla ya kumaliza mchezo.
Matokeo yanamaanisha, Azam sasa itabaki na pointi 53 na mechi mbili, ukiacha hiyo ya marudio na Mtibwa, pia watacheza na wakata miwa wengine, Kagera Sugar.

SOURCE: BIN ZUBEIRY (http/www,bongostaz.blogspot.com)

Comments

  1. Ni vituko katika soka letu ila hakuna jinsi mechi irudiwe tu kuepusha malumbano zaidi ila TFF wajipange.
    Mdau
    Mike

    ReplyDelete

Post a Comment