AZAM FC KUSHIRIKI KOMBE LA KAGAME



WASHINDI wa Medali ya Fedha ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC watashiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame Julai, mwaka huu, Dar es Salaam, imeelezwa.
Kuingia kwa Azam kwenye michuano hiyo, iliyofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1974, kunamaanisha Tanzania Bara, wenyeji watawakilishwa na timu tatu, nyingine zikiwa ni mabingwa watetezi wa Kombe hilo, Yanga na mabingwa wa Ligi Kuu, Simba SC.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah Malabeja amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba maandalizi ya michuano hiyo, yanaendelea vizuri na tayari wadhamini wamekwishapatikana na watatangazwa katika Mkutano maalum hivi karibuni.

Comments