MPYAA:ALI MAYAY NAYE TEMBELE AJIVUA GAMBA YANGA

MJUMBE wa kamati ya utendaji ya klabu ya Yanga Ali Mayay Tembele ameandika barua ya kujiuzulu nafasi hiyo. Mayay amefikia hatua hiyo kufuatia hali ya sintofahamu inayoendelea ndani ya klabu hiyo. Mayay ambaye alipata kuichezea Yanga na timu ya Taifa kwa mafanikio miaka ya nyuma, alisema anawajibika kufanya hivyo kama kiongozi kutokana na kutoridhishwa na mwenendo mzima wa klabu hiyo. Mayai anakuwa kioingozi wa nne kujiuzulu chini ya uongozi wa mwenyekiti Lloyd Nchunga ambapo awali alianza makamu Mwenyekiti, Davis Mosha, kisha akaja Sarah Ramadhan na baadaye Seif Ahmed

Comments