ZFA YAFUNGIA WAAMUZI WANNE, MOROCCO KUINOA ZANZIBAR HEROES

KAMATI ya utendaji ya Chama cha soka Visiwani Zanzibar (ZFA)kimemteua Hemed Moroco kuwa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar
‘Zanzibar Heros’ ambayo itashiriki mashindano ya nchi zisizo wanachamawa FIFA( VIVA) itakayoanza kutimua vumbi mei 29 nchini Kurdiftan.

Ofisa habari wa ZFA Munir Zakaria, amesema leo  kwamba kikao hichokilichoketi juzi visiwani humo, pamoja na Moroco kiliwateua HafidhMohamed kuwa kocha msaidizi, huku meneja wa timu na atakuwa Hasaa Hamis na daktari atakuwa Mohamed Mwinyi.
Aliongeza kuwa kamati hiyo pia imemteua Mohammed Ayoub kuwa kocha wa timu ya taifa ya vijana ‘Karume Boys’ ambapo atasaidiwa na Sheha
Hamis na daktari atakuwa Hamis Bilal.
Munir aliongeza kuwa tayari kamati ya utendaji ya ZFA imeshawaandikiabarua za kuwajulisha juu ya uteuzi huo.
Katika hatua nyingine, ZFA imewafungia mwaka mmoja waamuzi wannekuchezesha mechi zitakazofanyika katika visiwa hivyo kutokana na
nidhamu.
Munir alisema kati ya waamuzi hao wawili wana beji zinazotam,buliwa
na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Ramadhan Kibo na Mgaza
Kinduli, huku wengine ni Aamadhan Ally na Mohamed Kassim.

“Kamati imemua kutoa maamuzi hayo baada ya kubaini utovu wa nidhamu
hivyo imeona ni bora iwafungie waamuzi hao”, Alisema

Comments