YANGA YAGOMA KUPOKWA POINTI

KLABU ya soka ya Yanga imepinga kupokonywa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu na kamati ya Ligi ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF)
iliyokutana juzi jijini Dar es Salaam na kuipa klabu ya Coastal Unionya Tanga.
Kamati hiyo imefikia hatua hiyo kutokana na Yanga kumchezeshamchezaji Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kwenye mechi kati ya timu hizo iliyochezwa Machi 31 mwaka huu Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga,
ambapo Coastal ilipinga kuchezeshwa kwa Cannavaro ambaye alikuwaakitumikia adhabu ya kutocheza mechi sita.
 Ofisa Habari wa Yanga Louis Sendeu amesema kuwa hawajaridhisha na maamuzi hayo kutokana na ukweli
kwamba kamati ya Ligi haikuwa na mamlaka ya kutoa uamuzi huo kwani kikanuni kamati ya Nidhamu na usuluhishi ndiyo ilipaswa kupiatia rufaa
hiyo.
Alisema wanasubiri maamuzi ya kikao cha kamati ya nidhamu na usuluhishi ya TFF kilichotarajiwa kufanyika jana jioni kwa ajili yakupitia rufaa inayohusiana na adhabu za wachezaji wa Yanga iliyotolewana kamati ya Ligi na ndipo watajua nini cha kufanya.
“Kwa sasa hatuwezi kuongea zaidi kwani tunasubiri maamuzi ya kikao cha kamati ya nidhamu na baada ya hapo tutajua nini cha kufanya…kwa kweli
tumejipanga ipasavyo,”Alisema Sendeu.
Awali,ofisa habari wa TFF Boniface Wambura alisema jana kwamba uamuzihuo ulifanywa na Kamati ya Ligi kwa kuzingatia Kanuni ya 25(f) ya Ligi Kuu ya Vodacom juu ya Udhibiti wa Wachezaji.
Kanuni hiyo inasema: “Ni lazima kwa klabu na wachezaji kutunza kumbukumbu za kadi. Klabu itakayomchezesha mchezaji mwenye kadi tatu
(3) za njano au kadi nyekundu itapoteza mchezo na timu pinzani itapewa ushindi wa pointi tatu (3) na mabao matatu (3), iwapo mchezaji atacheza akiwa haruhusiwi kucheza kwa ajili ya kadi tatu (3) za njano au kadi nyekundu timu yake itapoteza mchezo. Endapo klabu haina uhakika au inataka taarifa ya idadi ya kadi zake itaomba kwa maandishi
toka TFF.”
“Cannavaro alioneshwa kadi nyekundu kwa kosa la kupiga kwenye mechi kati ya Yanga na Azam iliyochezwa Machi 10 mwaka huu ambapo kwa mujibuwa Kanuni ya 25(c) ya Ligi hiyo anastahili kukosa mechi tatu. Mchezajiamekosa mechi mbili tu,”Alisema Wambura
Wambura aliongeza kuwa kamati hiyo pia imezipiga faini ya shilingi500,000 kila moja klabu za Coastal Union na Yanga kutokana namashabiki wake kutupa chupa za majini uwanjani wakati wa mechi hiyo.
Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 32(1).
“Kamati hiyo pia imemuondoa Kamishna wa mechi hiyo Jimmy Lengwe kwenye
orodha ya waamuzi kutokana na upungufu uliopo kwenye ripoti yake
ambapo baadhi ya matukio makubwa hakuyaripoti. Moja ya matukio hayo ni
kocha wa Coastal Union, Jamhuri Kihwelo kuzozana na mshambuliaji wa
Yanga, Hamis Kiiza”, Aliongeza Wambura.

Vilevile waamuzi wa mechi namba 151 kati ya African Lyon na Simba
wameandikiwa barua ya onyo kwa kupata alama za chini. Waamuzi hao ni
Hashim Abdallah, Abdallah Selega, Hamis Chang’walu na Hassan Mwinchum.
Naye Kamishna wa mechi namba 153 kati ya Moro United na Villa Squad,
Arthur Mambeta amepewa onyo kutokana na upungufu katika ripoti yake.

Comments