YANGA WAZIDI KUMKABA KOO NCHUNGA NA WENZAKE

MAMBO ndani ya klabu ya Yanga yameendelea kuwa kizungumkuti baada ya baadhi ya wanachama kumtaka Mwenyekiti wa klabu hiyo Lloyd Nchunga ang'atuke madarakani, kuwa ndiye chanzo cha timu hiyo kufanya katika mechi zake za Ligi Kuu soka Tanzania Tanzania Bara.
Hatua hiyo inafuatia timu hiyo kupoteza mwelekeo katika mechi zake za Ligi hiyo katika siku za hivi karibuni  ambapo ilipokea vipigo viwili mfululizo na hivyo kujikuta  wakipoteza matumaini ya kuwania hata nafasi ya pili ambayo itawawezesha kushiriki michuano ya kimataifa mwakani. 
Baadhi ya wanachama wallisema wameiambia mamapipiro blog  kwamba Nchunga na kamati nzima ya utendaji ya klabu hiyo haina budi kujiuzulu ili kuepuka dhalili katika siku za baadaye.
“Hakuna haja ya kulitupia lawama benchi la Ufundi  kwani Mwenyekiti ndiye aliyeliteua hivyo ni yeye anatakiwa awajibike na si viongozi wa benchi la ufundi”, Alisema mmoja ya wanacha aliyejitamnbulisha kwa jina la Ismail Shaban.
Aidha, Ismail ambaye ni mwanachama wa Tawi la kariakoo akiwa ni Makamu Mwenyekiti wa kundi la ushangiliaji la Yanga Sapoti.alisema kuwa Nchunga alipaswa kuwajibika tangu timu ilipopokwa pointi tatu na mabao matatu na kamati ya ligi ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) na kupewa  Coastal Union ya Tanga.
Alisema kama angekuwa kiongozi makini asingeruhusu beki wao Nadir Haroub 'Cannavaro' acheze na matokeo yake baada ya kuona mambo yanakwenda vibaya ameamua kuwatoa kafara wengine.
"Nasema hivi tutaendelea kumkumbuka sana Makamu wetu Davis Mosha, kwa kuwa msimu uliopita tulishapoteza mwelekeo lakini kwa jitihada za Mosha tuliweza kutwaa ubinghwa katiukja hali ambayo haikutarajiwa.
Mwanachama mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Abdul  Nassoro (kadi namba 230), alisema kuwa Nchunga anatakiwa awe wa kwanza kung'atuka  kwani yeye ndiye aliyeifikisha Yanga hapa ilipo.
"Hata wachezaji wenyewe hawana nidhamu na viongozi wamekuwa mstari wa mbele kubariki madudu ya wachezaji na kuwatetea pale wanapokosea, kama baba hana nidhamu lazima na mtoto atafuata tabia ya baba…Nchunga aondoke kwa hiari yake yeye pamoja kamati zake alizounda kwani wameshindwa kuinusuru timu ," alisema Abdul.
Naye Mwanachama Mohamed Bakari wa Yanga Bomba, alimtaka Nchunga kuitisha mkutano wa dharura ili uongozi uweze kujibu maswali kutoka kwa wanachama wake.
Aidha Mwanachama mwingine wa Yanga Hussein Makabuleta naye aliutaka uongozi wa Yanga kujiondoa madarakani ili kuachia wengine kuongoza klabu hiyo kwa lengo la kuiletea mafaniki.

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHApril 21, 2012 at 4:42 AM

    hao wanachama waache uhuni,huyo mohammmed bakari sijui ndio nani,sisi kama bomba hatumjui mtu mwenye jina hilo,hivi uongozi huu ambao umetwa ubingwa wa africa mashariki na kati na vikombe vingine kibao uhukumiwe kwa kukosa ubingwa mwaka huu tu na tena timu bado ikiwa nafasi ya tatu au wana lao jambo hao wahuni...nchunga atabaki kuwa kiongozi mwenye mafanikio zaidi kwa miaka hii karibuni,kwani kaipa yanga ubingwa kwenye michuano ya kimataifa

    mdau wa bomba,revere,massachessetts

    ReplyDelete

Post a Comment