YANGA WAENDA MWANZA BILA PAPIC

MABINGWA watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga, wamekwenda jijini Mwanza bila ya kocha wao mkuu Kostadin Papic, imefahamika.
Yanga imekwenda huko kwa ajili ya mechi yake ya ligi hiyo dhidi ya wenyeji Toto Africans itakayopigwa wikiendi hii.
Taarifa zinasema kwamba Papic ameshindwa kuambatana na kikosi hicho kutokana na kuugua na kama hali yake ikitengemaa anatarajiwa kuungana na wachezaji wake kesho.
Ofisa habari wa Yanga Louis Sendeu amesema kwamba timu hiyo itatua kwanza Kahama, Shinyanga kwa ambapo kesho kitacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Kahama 2010 Fc.

Comments