YANGA SC WAPIGWA DONGO BUNGENI


NAIBU Spika wa Bunge, Job Ndugai ameipongeza klabu ya soka ya Simba kwa kusonga mbele kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF).
Aidha, Ndugai aliipiga kijembe timu pinzani ya Simba nchini Yanga baada ya kusema kuwa “Simba ni tofauti na timu nyingie zinazofanya vibaya kwenye michuano ya kimataifa”.
Kauli hiyo ililifanya bunge kuripuka kwa shangwe na  hasa wabunge mashabiki wa Simba kushangulia kwa kupiga meza.
Ndugai alitoa pongezi hizo baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu ,
“Nimeambiwa Simba ndiyo klabu pekee iliyosonga mbele katika nchi za Afrika Mashariki na Kati imetuletea sifa kubwa tofauti na klabu nyingine ambnayo imekuwa haifanyi vema kwenye mashindano ya kimataifa
Aidha aliwataka wachezaji wa timu hiyo kujiandaa na mechi yao dhidi ya                                Al Ahly Shandy ya Sudani ili iweze kufanya vizuri na hatimaye kusonga mbele.

Comments