YANGA NIPENI CHANGU NISEPE:PAPIC

LICHA ya uongozi wa Yanga kusisitiza kutodaiwa chochote nma kocha mkluu wa timu hiyo Kostadin Papic, kocha huyo amefunguka na kuutaka uongozi umlipe malimbikizo ya mshabara wake.
Papic amefikia hatua hiyo baada ya mkataba wake kutarajiwa kumalizika Aprili 24 mwaka huu huku uongozi ukiwa hauna mpango wa kumuongezea mkataba mpya.
Hata hivyo Papic alisema hatokuwa na kinyongo kama uongozi hautompa mkataba mpya lakini hatokuwa tayri kuondoka nchini bila ya uongozi kumlipa malimbikizo yake hayo ambayo yalisema yanafikia miezio mitatu.
Hii ni mara ya pili kwa Papic kuanika madai yake ya mshahara ambapo hivi karibuni alitangaza kuidai Yanga mshahara wa miezi mitatu kabla ya uongozi kukanusha na kusema kuwa kocha huyo ni muongo anaweka shinikizo la kutaka aongezewe mkataba.

Comments