WASANIIWA BONGOFLAVA WAPEWA DARASA

 Makamu     wa Rais wa Shirikisho la Muziki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha     muziki wa asili nchini, Che Mundugwao akiongea na wadau wa Jukwaa la Sanaa     (hawako pichani) wakati akiwasilisha mada iliyohusu Utunzi na Ubora Katika     Tungo za Muziki. Kulia ni Maafisa kutoka BASATA, Aristide Kwizela na Agnes     Kimwaga.
 Mkongwe     wa Muziki wa dansi nchini, Mzee Kassim Mapili akichukua notisi ya kile     kinachojadiliwa kwenye Jukwaa la Sanaa. Aliwaasa Wasanii kujifunza na     utumizi wa ala katika muziki.
Mdau     wakichangia mjadala kwa hisia.

Na Mwandishi Wetu
Wasanii wa muziki wa kizazikipya wameshauriwa kuwa na msimamo katika aina ya mahadhi ya muziki wanaoimbakuliko ilivyo sasa ambapo wengi wamekuwa wakichanganya na kushindwa kueleweka.
Wito huo umetolewa wiki hiina wadau wa Sanaa wakati wakiongea kwa nyakati tofauti kwenye Jukwaa la Sanaalinalofanyika kila wiki makao makuu ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambapowalisema kuwa, halil hiyo imeufanya muziki wetu ukose utambulisho na kushindwakufanya vizuri kimataifa.
“Wasanii wetu wamekuwawakichanganganya mahadhi (aina) ya muziki wanaoimba.Leo anaimba reggae, keshozouk mara muziki wa asili, hii inamfanya msanii asieleweke aina ya muzikianaoimba lakini pia tunakosa ubobezi kwenye aina hizi” alisema Che Mundugwaoambaye ni makamu wa Rais wa Shirikisho la Muziki nchini.
Aliongeza kuwa, kubadilika-badilikakwa wasanii kwenye aina ya muziki wanaoufanya si tu kumeufanya muziki wetuushindwe kuvuma kimataifa bali pia unakosa utambulisho kwenye aina zingine zamiziki zinazopatikana na kufahamika duniani kote.
“Muziki ni lugha ya Dunia,aina zake zinafahamika duniani kote.Tunachopaswa kufanya ni kutumia vionjo vyaasili yetu ili kuleta utofauti. Tusipofanya hivyo tutaendelea kuwatumbuizawatanzaia wenzetu waishio ughaibuni tu na si kufanya matamasha ya kimataifa”alisistiza Che Mundugwao ambaye pia ni msanii wa muziki wa asili.
Mdau mwingine aliyefahamikakwa jina la Mbile Hango alionya kuwa, wasanii wetu wataendelea kuvuma kwa mudamfupi na kutoweka kama hawatazingatia taaluma na ubobezi katika aina fulani yamuziki.
Aliongeza kuwa, ni vigumukwa wasanii kuimba kwa kunakiri muziki kutoka nchi za nje kama ile ya qwaitoyenye asili ya Afrika Kusini halafu wategemee kupata fursa ya kuuza kazi zaonje na kushiriki matamasha ya kimataifa.
“Ukinakiri muziki kutokanje maana yake huna kipya cha kupeleka nje, tutaendelea kuvuma humu humu ndani”alionya.
Mjadala wa wiki hii kwenyeJukwaa la Sanaa ulijikita kwenye Ubora katika Utunzi wa Tungo za Muziki

Comments