WAISLAMU WAMNYOOSHEA KIDOLE LULU

SIKU chache baada ya kufikishwa mahakamani kwa msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael 'Lulu' kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha msanii mwenzake Steven Kanumba, waislamu wamelaani msanii huyo kutoka mahakamani akiwa amevalia vazi la Hijab.
Tamko hilo lililotolewa jana katika msikiti wa Ngazija jijini Dar es Salaam wakati wa Swala ya Ijumaa ambapo waumini hao walidai kuwa msanii huyo anaudhalilisha uislamu.
Walisema hawakupendezwa na kitendo hicho na kama atapandishwa tena mahakamani katika mavazi hayo wataandamana.

Comments