VILLA SQUAD YAOMBA MSAADA

TIMU ya soka ya Villa Squad imeomba wadau mbalimbali kujitokeza kuisaidia timu hiyo ili iweze kufanya maandalizi yake ya mechi zilizosalia kwenye ligi kuu soka Tanzania Bara.
Katibu mkuu wa klabu hiyo Frank Mchaki amesema kwamba timu hiyo haina mfadhili hivyo inawawia vigumu kufanya kikamilifu maandalizi ya michezo yake.
Timu hiyo leo inashuka katika dimba la Chamazi jijini Dar es Salaam kukwaana na Coastal Union ya Tanga

Comments