UONGOZI RUVU SHOOTING WASHIKA UCHAWI WACHEZAJI KIPIGO CHA SIMBA

KIKOSI CHA RUVU SHOOTING

UONGOZI wa timu ya soka ya Ruvu Shooting ya mkoani Pwani umesema kwamba uzembe wa nyota wake Mohammed Kijuso na Abdallah Juma ndio ulipelekea timu hiyo kupata kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Simba.
Timu hizo zilikwaana katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa ligi kuu soka tanzania Bara ambapo bao la Simba lilifungwa na Patrick Mutesa Mafisango na hivyo kuifanya Simba iendelee kukalia kiti cha Ligi hiyo hiyo ikifikisha pointi 53.
 Ofisa habari wa Ruvu Shooting ameimbia mamapipiro blog kuwa kuwa  kufanya kwao vibaya katika mchezo huo kulichangiwa na wachezaji hao ambao walionekana kutokuwa makini dimbani hali iliyowafanya washindwe kufunga mabao.
Alisema licha ya kupata nafasi za wazi wachezaji hao walishindwa kuzitumia vema nafasi nyingi za wazi walizozipata na hivyo kujikuta timu ikikosa mabao zaidi ya matatu.
“Kwa kila aliyeutazama mchezo ule atakubali kuwa tuliwazidi kimchezo Simba katika kila idara lakini tuliangushwa na safu ya ushambuliaji na hasa Juma na Kijuso kwa kweli wametukosesha ushindi kizembe kabisa,”Alisema.
Aliongeza kuwa baada ya mchezo huo kocha wao mkuu Charles Boniface Mkwasa atayafanyia marekebisho mapungufu yaliyojitokeza ili iweze kufanya vema katika mchezo wao unaofuata dhidi ya Moro United keshokutwa.

Comments