U-20 ZA SIMBA NA AZAM FC KUMENYANA J'MOSI CHAMAZI






TIMU za vijana wenye umri chini ya miaka 20 za Azam Fc na Simba keshokutwa zinatarajiwa kukwaana katika dimba la Chamazi ikiwa ni mchezo maalum wa kuadhimisha kifo cha rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Aman Karume.
 Msemaji msaidizi wa Azam Fc Jaffer Idd Maganga alisema maandalizi kwa ajili ya mchezo huo yanakwenda vizuri. 
Alisema timu hizo ambazo zimekuwa zikichuana vikali katika michuano mbalimbali ya Vijiana ikiwemo ile inayoshirikisha timu za Vijana  ‘Uhai Cup’ ambapo Simba inashikilia ubingwa. 

Comments