TUMBO LAMKOSESHA SUNZU NA MAAFANDE


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Simba Felix Sunzu jana alishindwa kuitumikia timu yake katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya maafande wa Ruvu Shooting kutokana na kuumwa tumbo.
Sunzu ambaye kwa kiasi kikubwa amekuwa akichangia mafanikio kwa timu yake alishindwa kucheza mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la taifa baada ya hali yake kuwa mbaya hivyo kulazimika kukaa nje ya dimba.
Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga alisema kwamba kwa sasa nyota huyo anaendelea vema baada ya kupata matibabu na kama hali ikiendelea kuwa vizuri jumatano ataitumikia timu hiyo katika mchezo wake na Moro United.
Katika mchezo huo Simba ilishinda bao 1-0 na hivyo kufikisha pointi 53 huku ikiendelea kukalia kiti cha ligi hiyo ikifuatiwa na Azam Fc yenye pointi 50 na Yanga inayoshika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 47.

Comments