TIBAIGANA KUTOA HATMA YA POINTI TATU ZA YANGA LEO

KAMATI ya nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) chini ya Mwenyekiti wake kamishna mstaafu wa jeshi la Polisi Alfred Tibaigana,  inakutana jioni ya leo kwa ajili ya kujadili rufani ya klabu ya soka ya Yanga iliyowasilishwa kwa kamati hiyo ikipinga kupokwa pointi tatu na mabao matatu.
Kamati ya Ligi ya TFF iliipoka Yanga pointi na mabao hizo na kuzipeleka kwa klabu ya Coastal Union ya Tanga baada ya Yanga kumtumia beki wake Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye alikuwa anatumikia adhabu ya kadi.
Katika mchezo baina ya Yanga na Coastal uliopigwa kwenye dimba la Mkwawani, Tanga, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Comments

Post a Comment