TIBAIGANA KUAMUA POINTI TATU ZA YANGA J'MOSI


Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inatarajia kukutana Jumamosi (Aprili 14 mwaka huu) kujadili rufani ya Yanga inayopinga kunyang’anywa pointi tatu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Alfred Tibaigana
Kamati ya Ligi ya TFF iliinyang’anya Yanga pointi tatu ilizopata kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Coastal Union kwa kumchezesha beki Nadir Haroub anayetumikia adhabu ya kukosa mechi tatu.

Comments