TBF YAWAFUGULIA WACHEZAJI WA MWANZA, VIONGOZI KUENDELEA NA KIFUNGO


SHIRIKISHO la Mpira wa Kikapu Tanzania(TBF) limewafungulia wachezaji wa timu hiyo na kubakiza adhabu kwa viongozi.
Rais wa TBF Musa Mziya alisema kuwa wameawafungulia wachezaji hao baada ya kuandika barua ya  kukiri kosa na kudai kuwa lilisababishwa na viongozi walioambatana na timu kuwashawishi wachezaji kuvunja kanuni za mashindano.
Alisema kuwa pamoja na kuondoa adhabu hiyo TBF imewataka wachezaji hao kulipa faini ya sh 300,000 kabla ya kuanza kushiriki shughuli zozote za mpira wa kikapu.
“kamati ya utendaji inautaka mkoa wa mwanza kuendelea kujitafakari katika nidhamu na uvunjaji wa amani ya mchezo,na TBF itakuwa inasimamia na kuhusika kwa kipindi cha mwaka mmoja wa adhabu kwa kaimu mwenyekiti MRBA Kizito Bahati,Robert Mwita ambaye ni kocha na kocha msaidizi Amri Mohamed”alisema Mziya

Comments