TANZANIA ALL STARS KUKIPIGA NA HARAMBEE STARS KESHO

WACHEZAJI wa zamani wa timu ya Taifa (Tanzania All Stars) wameondoka kwenda nchini Kenya kwa ajili ya kucheza mechi za kirafiki na timu ya Taifa ya Kenya 'Harambee Stars'
Kocha wa timu hiyo Kitwana Manara alisema jana kwamba mchezo wa kwanza utafanyika kesho huko Mombasa, kabla ya kumenyana tena Mji wa Malindi na nyingibne kupigwa mjini Lamu.
Alisema kisi cha wachezaji 22 akiwemo yeye kitaondoka leo na kusema kuwa wamwejipanga vema kuhakikisha wanashinda michezo yao hiyo.
Baadhi ya wachezaji wanaounda kikosi hicho ni pamoja na Nassoro Mrisho, Edibily Lunyamila, Abdallah Kibaden, Lawrance Mwalusako, David Mwakalebela, Omar Gumbo, Madaraka Suleiman, Makumbi Juma, Sekilojo Chambua na wengineo.

Comments