SIMBA YASONGA MBELE AFRIKA, SETIF OUT, OKWI SHUJAA


Simba SC
SIMBA SC imefuzu kuingia Raundi ya Tatu ya Kombe la Shirikisho la Soka CAF, kwa faida ya bao la ugenini baada ya kufungwa mabao 3-1 na ES Setif kwenye Uwanja wa Mei 8, mjini Setif katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Shukrani kwake mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi aliyefunga bao la dakika za lala salama wakati refa amekwishaonyesha dakika za majeruhi tano.
Katika mchezo huo, Simba ilipata pigo mapema dakika ya 18 baada ya beki wake Juma Said Nyosso kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kucheza ‘rafu ya wazi’.
Hadi mapumziko, tayari Setif walikuwa mbele kwa mabao 2-0 na mapema kipindi cha pili, wakapiga la tatu.
Mchezo wa kwanza Simba ilishinda 2-0 Dar es Salaam na sasa itamenyana na Al Ahly ya Sudan.

Comments

  1. Simba wacheka kama kibelala.....mhhhh......aaaahhh.......mhhhh......aaaahhh,weekend yetu itakuajema eee,simbaaaaaaa!

    ReplyDelete

Post a Comment