SIMBA WAAGIZA MSOSI KUTOKA BONGO

KATIKA kujihadhari na hujuma klabu ya soka ya Simba imeamua kuagiza mchele, maharage, maji na matunda kutoka Tanzania.
Simba kwa sasa ipo nchini Algeria kujiandaa na mchezo wake wa marudiano wa Kombe la Shirikisho (CAF) dhidi ya Es Setif ya huko unaotarajiwa kupigwa wikiendi hii nchini humo.
Mwenmyekiti wa Simba aliyeko huko amesema kuwa wameamua kuchukua tahadhari hiyo baada ya kukumbana na vitendo vya hujuma pindi waluipotua nchini humo.
Alisema wapinzani hao wamepanga kuwahujumu kwa namna moja ama nyingine ili kuhakikisha wanashinda mechi hiyo na kusema kuwa wamejipanga kukabiliana na hila za waarabu hao na timu inaendelea vema na maandalizi ya mchezo huo.

Comments