SIMBA SC WARUDI CHIMBO KUSAKA DAWA

VINARA wa ligi kuu soka Tanzania Bara jioni ya leo wanatarajiwa kurejea kambini tena kwa ajili ya kujiandaa na mechi yao dhidi ya JKT Ruvu.
Simba ambayo jana iliibamiza Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi hiyo ambapo wachezaji walipewa mapumziko ya siku moja, itarejea tena katika kambi yake iliyopo Bamba Beach jijini Dar es Salaam.
Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kwamba kikosi hicho kitaingia kambini mara baada ya mazoezi ya jioni yatakayofanyika katika uwanja wa TCC Chang'ombe.

Comments