SIMBA SC WAANZA KUSAKA MAKALI YA VPL

BAADA ya kutinga hatua ya 16 bora ya kombe la Shirikisho barania Afrika (CAF), klabu ya soka ya Simba imeanza rasmi mazoezi leo kujiandaa na michezo ya ligi kuu ya Vodacom.
Simba ilitinga hatua hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuitoa ES Setif ya Algeria kwa mabao 3-3 huku ikibebwa na bao la ugenini kwani katika mchezo wa awali ilishinda mabao 2-0, kabla ya kufunga mabao 3-1 katika mechi ya marudiano iliyopigwa nchini Algeria.
Kwa kuvuka hatua hiyo Simba sasa itakutana na Al Ahly ya Sudan mwishoni mwa mwezi huu kwa mchezo wa kwanza kupigwa nyumbani.
VInara hao wa VPL leo asubuhi walifanya mazoezi ya viungo 'GYM' huku jioni wakitarajiwa kufanya mazoezi ya kawaida katika viwanja vya TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam.

Comments