SIMBA RAHAAA UTAMU, YANGA MWAKA WA TABU



Wekundu wa Msimbazi wameendelea kunusa ubingwa wa Ligi kuu ya Vodacom baada ya kushinda mabao 3-0 dhidi ya JKT Ruvu na hivyo kuendelea kukalia kiti hicho baada ya kufikisha pointi 56 katika msimamo wa ligi.


Kama wanavyoonekana wachezaji wa Simba kutoka kulia ni Gervas Kago, Patrick Mafisango na Uhuru Selelani wakishangilia baada ya goli la kwanza katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa, ambapo mabao ya  Simba yalipachikwa na Uhuru Selemani,Mwinyi Kaizimoto na Haruna Moshi Boban.
 
 
Aidha mahasimu wa Simba timu ya Yanga leo wameendelea kuzika ndoto za kutetea ubingwa baada ya kutandikwa bao 1-0 na timu ya Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kaitaba huko Bukoba mkoani Kagera, mbali na mechi hizo kulikwa na michezo mingine ambapo Toto Africa imeifunga Africa Lyon mabao 3-0 kwenye uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza huku Coastal Union ikiitandika Polisi Dodoma mabao 3-1 na Ruvu Shooting ikiifunga ikiifunga Moro United bao 1-0.
Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia kwa nguvu baada ya timu yao kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu JKT kwenye uwanja wa Taifa leo.

Comments