SHANDY NI SALAMU KWENU YANGA

BAADHI ya mashabiki wa klabu ya Soka ya Simba wamejitapa kuwa kipigo  cha mabao 3-0 walichowapa Al Ahli Shandy ya Sudan juzi ni salamu kwa mahasimu wao  jadi nchini Yanga ambao watakutana nao jumamosi ijayo katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara.
wakizungumza mara baada ya mchezo baina ya Simba na wasudan hao uliopigwa jana kwenye dimba la Taifa jijini dar es Salaam, mashabiki hao walisema baada ya Wasudan hao sasa inakuja zamu ya Yanga.
Moto huu tuluiouwasha kwa Shandy unaelekea sasa kwa Yanga Jumamosi hivyo wasubiri kuipigo kitakatifu, "aliswema Shabiki mmoja wa Simba.
Shabiki mwingine wa Simba aliimbia mamapipiro blog kwamba kiwango ilicho nancho Simba kwa sasa hakuna timu inayoweza kuifikia kwa sasa hivyo timu zote watakazokutana nazo zisubiri kupokea mvua ya magoli.
Simba ilikutana na Shandy katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya kombe la Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) imepania kulipiza kisasi cha kufungwa baio 1-0 na Yanga katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo.

Comments