SAJNA ADONDOSHA PINI JIPYA 'MWANANGU'


Tetemesha Records inamleta kwa mara nyingine msanii SAJNA na safari hii amemshirikisha msanii wa kike anaitwa VUMILIA aliewahi kufanya vizuri na nyimbo kama (Utanikumbuka) na nyingine nyingi. Wimbo huu mpya wa SAJNA unaitwa "MWANANGU".
Huu ni wimbo ambao unazungumzia mapenzi ya mzazi kwa mwanae, na umelenga pande zote yaani mzazi wa kike na mzazi wa kiume, pia mtoto wa kike na mtoto wa kiume. Lakini pia hata wale ambao hawajapata watoto hawakusahaulika. Hivyo kwa mantiki hii ni wimbo unaomgusa kila mmoja katika jamii. 

Song details
 Track Name: MWANANGU
Artists: SAJNA ft. VUMILIA
Lyrics composed by: SAJNA, JOSEFLY & KID BWOY
Arranged by: KID BWOY
Produced by: KID BWOY & AMBA
Mixed by: KID BWOY
Studio: TETEMESHA RECORDZ
April 2012

Comments