SAA NAO WAMLILIA STEVEN KANUMBA

CHAMA cha washereheshaji (SAA) kimetuma salamu za rambirambi kwa wasanii wa Bongo Muvi kufuatia kifo cha msanii mwenzao Steven Kanumba aliyefariki usiku wa kuamkia jumamosi nyumbani kwake Sinza, Vatican.
Mlezi wa Saa, Mc Mdachi (pichani) amesema kwamba kifo cha KAnumba si pengo tu kwa sawanii hao bali ni kwa Watanzania wote kutokana na mchango mkubwa alioutoa marehemu ambao umeweza kuitangaza Tanzania nje ya mipaka kupitia sanaa.
"tumemnpoteza mwanasanaa mwenzetu katika filamu ambaye alijibidiisha kukuza vipaji vya wasanii wadogo nchini na kuonyesha njia kwa wengine,"Alisema.
RAHA YA MILELE MPE EE BWANA, PUMZIKA KWA AMANI KANUMBA!

Comments