SAA CHACHE KABLA YA KUWAVAA MAAFANDE SIMBA WAHAMISHA KAMBI

VINARA wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba wamehamisha kambi yao kutoka hoteli ya Bamba Beach iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam na kuhamia katikati ya jiji.
Habari ambazo mamapipiro Blog imezinasa zinasema kwamba wekundu hao wa Msimbazi wamejichimbia katika hoteli moja (jina kapuni) kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao wa ligi dhidi ya JKT Ruvu unaotarajiwa kupigwa kesho katika dimbna la Taifa jijini Dar es Salaam.
Kumekuwepo na taarifa kuwa Simba imeamua kutimka Bamba kutokana na kuepuka kufanyiwa hujuma kutokana na ukweli kwamba mchezo wa kesho ni mgumu hivyo wameona ni vema kuchukua tahadhari kapbka ya hatari.
Hata hivyo mmoja ya viongozi wa Simba aliimbia blogu hii kwamba ni jambo la kawaida kwa timu hiyo kuhamia katikati ya jiji saa chache kabla ya kucheza mechi zake.
Simba inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 53.

Comments