RUVU SHOOTING WATAKA SHERIA 17 KUZINGATIWA KESHO

WAKATI kesho inashuka katika dimba la Taifa jijini kukwaana na vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba, maafande wa Ruvu Shooting wameomba mwamuzi wa mchezo huo kufuata sheria 17 za soka.
Msemaji wa maafande hao Masau Bwire ameiambia mamapipiro blogu kwamba wameamua kutoa hadhari hiyo kutakana na kuhisi kuwepo kwa ukiukwaji wa sheria hizo katika mchezo wa kesho.
"Kikosi chetu kipo kamili kwa ajili ya mchezo wa kesho na wachezaji wana ari kubwa, lakini tunapenda kusisitiza waamuzi kufuata sheria 17 za soka ili mshindi apatikane lkwa haki,"Alisema Bwiure.
Alisema wamefanya maandalizi makubwa kuhakikisha wanashinda mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na upinzani mkali.
Aliongeza kuwa katika kuhakikisha wachezaji wanashinda mchezo huo uongozi wa timu hiyo jioni ya leo unatarajiwa kukutana na wachezaji wa timu hiyo kwa lengo la kuwajaza morali.

Comments