RUTASHOBORWA KUAGWA JUMATATU IJAYO


MWILI wa mjumbe wa kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga Theonest Rutashoborwa (pichani)unatarajiwa kuagwa jumatatu ijayo katika kanisa katoliki parokia ya kijichi kabla ya kusafirishwa kwenda kwao kijiji cha Bukabaye kilicopo Bukoba mkoani Kagera.
Rutashoborwa ambaye kitaaluma ni wakili akimiliki kampuni ya Brilliance Law Chambers ya jijini Dar es Salaam alikutwa na umauti huo usiku wa kuamkia leo katika  hospitali ya Agha Khan alipokwenda baaada ya kujisikia vibaya kabla ya kubainika kuwa na kisukari na shinikizo la damu. 
Ofisa habari wa yanga, Louis Sendeu amesema kuwa Rutashoborwa alianza kujisikia vibaya mara alipotua uwanja wa ndege wa mwalimu Jk Nyerere akitokea Moshi, Kilimanjaro alipokwenda kwa shughuli zake za kikazi na alipokimbizwa hoispitalini alifariki akiwa katika harakati za kupelekwa chumba cha uangalizi maalum (ICU). 
“Yanga inasikitisha kumpoteza kiongozi huyu hidari ambaye alikuwa muhimili mkuu katika kuinganisha Yanga, kwa nianba ya wanachama na wapenzi wa Yanga tunatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu jamaa na marafiki,”Alisema Sendeu.
“Marehemu ameacha mjane na watoto wanne, bwana ametoa Bwana ametwaa, mwenyezi mungu aiweke rioho ya marehemu mahali pema peponi, Amin,”Alisema.

Comments