ROONEY AWAKARIBIA MAGWIJI MAN U




MSHAMBULIAJI Wayne Rooney akiwa katika kiwango cha juu Manchester United inayowania taji la 20 la Ligi Kuu  yuko katika nafasi ya kuingia kwenye orodha ya wafungaji wa kihistoria wa mabao wa timu hiyo.
United imewaacha kwa pointi tano wapinzani wao Manchester City, huku Rooney akiwaokotesha mipira nyavuni makipa mara nane katika mechi saba zilizopita, hivyo kutimiza mabao 28 katika mashindano yote msimu huu na 175 kwa ujumla.
Kuelekea mechi na Queens Park Rangers Jumapili Uwanja wa Old Trafford, Rooney anazidiwa mabao manne tu na George Best na Dennis Viollet, ambao wanalingana katika nafasi ya tatu katika orodha ya wafungaji bora wa kihistoria wa United.
Kama United itashinda mechi ya nane mfululizo ya ligi, City itakwenda kuvaana na Arsenal wanaoshika nafasi ya tatu baadaye Jumapili hiyo ikiwa inazidiwa pointi nane

Comments