ROBBEN KUONGEZA MKATABA BAYERN


Robben

WINGA Mholanzi wa Bayern Munich, Arjen Robben anajiandaa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuwatumia Tha Bavaria hadi utakapofanyika uchaguzi mwingine wa Tanzania, mwaka 2015, hiyo ni kwa mujibu wa gazeti la kila siku la Ujerumani, Bild leo.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye alisaini timu hiyo akitokea Real Madrid Agosti mwaka 2009, mkataba wake wa sasa ni hadi mwaka 2013, lakini kwa mujibu wa gazeti hilo la Ujerumani, atasaini kurefusha mkataba wake mwishoni mwa mwezi huu utakaomfanya aendelee kuishi Jiji la Munich kwa angalau miaka mitatu zaidi.
Anatarajiwa kusaini mkataba mpya baada ya mechi ya mwisho ya Bayern ya ligi nyumbani msimu huu dhidi ya VfB Stuttgart, Aprili 28.
Robben amekuwa kwenye kiwango kizuri  Bayern akifunga mabao 11 katika ligi ya Ujerumani na matatu katika Ligi ya Mabingwa.
Alifunga bao la ushindi dhidi ya Nuremberg Jumamosi, ambalo linaifanya Bayern ibaki inazidiwa pointi tatu na vinara wa Bundesliga, Dortmund.
Na bao lake la kipindi cha pili liliipa Bayern ushindi wa 2-0 katika Robo Fainali ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Marseille Jumatano iliyopita na kuitengenezea klabu hiyo ya Ujerumani mazingira ya kutinga Nusu Fainali kuelekea mechi ya kesho ya marudiano mjini Munich.
Kocha wa Bayern, Jupp Heynckes amesema leo kwamba anatarajia "kwamba Arjen atasaini " ofa huyo ya Munich hivi karibuni.
"Nafikiri ameonyesha tena ni kiasi muhimu kwa Bayern. Ni mchezaji wa timu. Ambayo inamfanya awe mchezaji mwenye thamani sana kwetu," alisema Heynckes.
Kumekuwa na taarifa kwenye vyombo vya habari Ujerumani siku za karibuni kuhusu maelewano mabaya kati ya Robben na Heynckes, na nyota huyo wa Uholanzi alisema amekaa sana benchi msimu huu.
Rais wa zamani wa Bayern, Franz Beckenbauer pia alimkandia Robben kwenye Televisheni.
Mwanzoni mwa Februari, Robben aliachwa kwenye kikosi kilichoshinda 2-0 dhidi ya Stuttgart katika Kombe la Ujerumani na pia akakosa mechi mbili nyingine za ligi akiwa benchi.
Robben alinukuliwa na gazeti la Uholanzi Nusport akisema kwamba alikuwa ana wakti mbaya sana akikaa benchi.
Leo, Heynckes ameyapuuza maneno hayo akisema kwamba hajayasikia moja kwa moja kutoka kwa Robben na kusema kwamba yuko vizuri sana na mchezaji huyo.

Comments