REY MYSTERIO ASIMAMISHWA WWE


NEW YORK, MAREKANI
NYOTA wa mieleka kutoka chama cha mieleka duniani (WWE), Oscar Gutierrez ‘Rey Mysterio’ amesimamishwa kwa muda wa siku 60 baada ya kufanya vurugu kwa mara ya pili katika mashindano ya Talent Wellness Program. 
Chama hicho kimetoa taarifa yake mtandaoni kikisema kwamba, "kwa makubaliano na waandaaji wa Talent Wellness Program, WWE imemsimamisha Rey Mysterio kuacha kucheza kwa muda wa siku 60, kwa kufanya kosa la vurugu. "
Kwa mujibu wa ripoti hiyo imesema mbabe huyo mwenye miaka 37, amechukuliwa uamuzi kutokana na kurudia kosa hilo alilowahi kulifanya mwaka 2009.

Comments