RASMI:MASHUJAA YAIBOMOA TENA TWANGA, YAMNYAKUA MCD,FER



BENDI ya Mashujaa Musica imeendelea kuibomoa African Stars ‘Twanga Pepeta’ ambapo safari hii imemyakua mpiga tumba wake nguli Sudi Mohammed ‘MCD’. 
Twanga pia imeibomoa Extra Bongo baada ya kumyakua rapa wake, Saulo John 'Ferguson'.
Meneja wa Mashujaa Musica King Dodoo aliiambia mamapipiro blog kuwa  wameamua kuwachukua wanamuziki hao ili kuimarisha bendi yao katika ushindani wa muziki ambapo wasanii hao wamejiunga kwa mkataba wa miaka miwili. 
Alisema pamoja na kuongeza nguvu katika bendi hiyo, wamewachukua wanamuziki hao kwa ajili ya kuendeleza vipaji vyao, ambapo Ijumaa hii wanatarajiwa kutambulishwa rasmi katika onyesho litakalofanyika kwenye ukumbi wa Busness Park, Kijitonyama jijini Dar es Salaam. 
Kwa upande wa wasanii hao kila mmoja alisema ameamua kujiunga na bendi hiyo kwa ajili ya kuendel;eza kipaji alichonacho sambamba na maslahi mazuri ambayo wamepewa na watakayopewa pindi watakapokuwa wakiitumikia bendi hiyo. 
“Kikubwa ni maslahi ndiyo yamenipeleka Mashujaa Musica kwani siku hizi kila mtu anaangali maslahi yake kwanza, pia nataka kuendeleza umahiri wangu katika upigaji tumba ,”Alisema MCD ambaye ameitumikia Twanga Pepeta kwa miaka 12. 
Naye Ferguson tayari ametunga vibao vitatu kwa ajili ya mashabiki huku pia akitarajia kutambulisha mtindo mpya uitwao ‘Kibega’

Comments