PAPIC MUONGO-YANGA

UONGOZI wa klabu ya Yanga umeshangazwa na taarifa za kuwa kocha wa klabu hiyo Mserbia Kostadin Papic anaidai klabu hiyo mshahara wa miezi mitatu.
Ofisa habari wa Yanga Louis Sendeu amesema habari hizo si za kweli kwani kocha huiyo amekuwa akilipwa mshahara wake kila mwezi.
Alisema nashangazwa na taarifa hizo za uongo ambapo hata walipomuuliza kocha huyo alikana kuongea na chombo chochote cha habari kuhusiana na taarifa hizo.
"Yaani sijui hizi taarifa zinatoka wapi hata Papic tumemuuliza anazikana...kiukweli kocha huwa analipwa chake kila mwanzo mwezi,"Alisema Sendeu.
Sendeu aliongeza kuwa kikosi hicho kilichopo mjini Kahama kwa mechi moja ya kirafiki jioni ya leo, kesho kitakwenda jijini Mwanza tayari kwa mechi yake ya ligi kuu bara dhidi ya Toto Africans ya huko itakayopigwa jumapili kwenye dimba la CCM Kirumba jijini humo.
Sendeu alisema kocha huyo ambaye hajaambatana na timu kutokana na kuugua tumbo na mafua huenda akaunga na kikosi kesho mjini Mwanza.

Comments