PAPIC AGEUKA BUBU, KIKOSI KAMILI CHATIA TIMU BUKOBA

KOCHA mkuu wa mabingwa watetezi wa ligi kuu bara Yanga, Kostadi papic jana aligeuka kuwa bubu baada ya timu yake kupokea kichapo cha mabao 3-2  dhidi ya Toto African ya Mwanza katika dimba la Taifa.
Kama ilivyoada baada ya mchezo kwa makocha kuzungumzia mpambano, lakini mambo yalikuwa kinyume kwa Papic ambaye aligoma kuzungumza na waandishi wa habari.
Kutokana na kipigo hicho Yanga imeendelea kushika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 43 nyuma ya Azam Fc yenye pointi 50 na vinara Simba wenye pointi 53.
Katika hatua nyingine, kikosi cha Yanga kimewasili mjini Bukoba tayari kwa mchezo wao wa ligi hiyo dhidi ya wqenyeji Kagera Sugar utakaopigwa jumatano katika dimba la kaitaba mjini Bukoba.

Comments