PAMOJA NA KUTAKIWA KUJIVUA GAMBA, VIONGOZI YANGA WASEMA BADO WAPO WAPO KWANZA

Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga wakati akiomba kura
BAADA ya badhi ya wanachama wa klabu ya Yanga kuutaka uongozi wa klabu ya Yanga kujiuzulu kutfuatia kufanya vibaya kwa timu hiyo kwenye ligi kuu soka Tanzania bara,uongozi wa umesema bado una tathmini tatizo ni nini.
Hatua hiyo inafuati jana timu hiyo kupokea kipigo cha bao 1-0 toka kwa Kagera Sugar hivyo kufanya timu hiyo kuweka rehani ubingwa wake iliokuwa ikiutetetea.
Kutokana na udhaifu iliyouonyesha timu hiyo, Mwenyekiti wa kamati ya Matawi ya Yanga, Mohammed Msumi aliutaka uongozi wa Yanga chini ya Mwenyekiti wake Lloyd Nchunga kujiuzulu kutokana na kushindwa kuiletea mafanikio timu hiyo.
 Akizungumza katika kituo kipindi cha michezo cha Redio One, Msumi alisema kuwa kuna haja ya viongozi hao kujiweka kando na timu hiyo baada ya kushindwa kutimiza ahadi zao walizoahidi pindi walipokuwa wanaomba kura toka kwa wanachama.
 “Kwa kweli tumesikitishwa na mwenendo mbaya wa timu wetu kwenye ligi kuu bara, hivyo uongozi hauna budi kuachia ngazi kwa sababu hakuna walichokifanya,”alisema Msumi.
Akizungumzia mtazamo huo wa Msumi, Mjumbe wa kamati ya Utendaji ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano ya Yanga Ali Mayai Tembele aliiambia mamapipiro Blog kwamba ni mapema mno kuamua kujiuzulu ama kutojiuzulu.
Alisema wanaheshimu maoni ya Msumi kama mwanachama wa Yanga lakini kabla ya uamuzi wowote kamati ya Utendaji haina budi kukutana na kutathmini kwa kiasi gani tumefanikiwa au kutofanikiwa ndipo tutawaeleza wanachama.
“Mzee wetu Msumi ana haki ya kusema kile anachokifikiria kutokana na hali halisi ilivyo lakini ni vigumu kwa mtu mmoja mmoja kufanya maamuzi ni lazima tukutane kama kamati na kujadili mambo yanavyokwenda,”Alisema Mayai.
Mchezaji huyo wa zamani wa Yanga na timu ya Taifa aliongeza kuwa hata uongozi pia umesikitishwa na mwenendo wa timu hiyo , hivyo hawanabudi kukaa chini na kuangalia tatizo ni nini.
Yanga ambayo inashika nafasi ya tatu kwenye ligi hiyo ikiwa na pointi 43 nyuma ya Azam yenye pointi 50 na Simba inayoongoza ligi hiyo iliwa na pointi 56, imeshafifisha ndoto zake za kuwania ubingwa huo.

Comments